Baada ya Mo Dewji, Lema aja na mengine matatu
0
November 01, 2018
Waziri Kivuli wa masuala ya mambo ya ndani ya nchi Gobless Lema amesema anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari juu ya madai ya kuwepo kwa mauaji ya raia na jeshi la polisi mkoani Kigoma eneo la Uvinza.
Kwa mujibu wa Lema licha ya kutotaja siku na muda husika ambao atazungumza, pia ameeleza kwenye mkutano wake huo atazungumzia hatua ya kukamatwa kwa Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe na kuhojiwa na jeshi la polisi jana kwa kutoa taarifa za ambazo zinatajwa ni tofauti na jeshi la polisi.
Aidha, Godbles Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini amesema atazungumzia hatua ya kukamatwa kwa ndugu wa mfanyabiashara Rostam Aziz anayefahamika kwa jina la Akram Aziz ambaye jana alifikishwa mahakamani kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali bila kuwa na kibali.
“Kwanza ninatoa pole kwa familia za Polisi na raia ambao ndugu zao wamepoteza maisha huko Mpeta Uvinza, nitaongea na vyombo vya habari kuhusu mauaji hayo na kukamatwa kwa Zitto Kabwe pamoja na sakata la mfanya biashara Akram Aziz” Amesema Lema
Mpaka sasa si jeshi la polisi au waziri husika ambaye amejitokeza kuzungumzia masuala hayo.
Mara kwa mara Mbunge huyo amekuwa akijitokeza kutoa maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni juu ya matukio yanayotokea nchini ambapo, oktoba 16 mwaka huu alijitokeza na kuzungumzia sakata la kupotea kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji.
Tags