Baba Mzazi Adakwa na Polisi kwa tuhuma za kumpa mimba bintiye

Baba Mzazi Adakwa na Polisi kwa tuhuma za kumpa mimba bintiye
Polisi mkoani Arusha wanamshikilia mkazi wa Sakila, Kata ya Kikatiti, wilayani Arumeru, David Nnko (73), kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita (jina la mwanafunzi na shule vinahifadhiwa).

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa matukio ya ubakaji na utiaji mimba yamekuwa mengi wilayani humo na katika miaka miwili iliyopita, wanafunzi 84 wa shule za sekondari na msingi wamekumbwa na tatizo hilo.

Alisema kutokana na vitendo hivyo kukithiri, serikali wilayani humo imeamua kushirikiana na viongozi wa vyombo mbalimbali kukabiliana na suala hilo kwa kuunda kamati maalum.

"Lakini wilaya yetu tumeamua kutenga wiki nzima kuanzia Jumanne ijayo tutapokea malalamiko ya wote waliobakwa na kupatiwa mimba kwa kipindi cha miaka mitano nyuma. Hata kama kesi zao ziko mahakamani au polisi waje kutueleza ili tuongeze nguvu zichukuliwe hatua za haraka," alisema.

Alisema mbali na kupokea malalamiko hayo mbele ya kamati maalum itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, James Nchembe, pia watawaonyesha hadharani watuhumiwa wote wa ubakaji ili jamii na dunia iwafahamu.

Muro alisema wilaya hiyo imekithiri matukio hayo kila siku lazima wapokee taarifa za masuala hayo, kitendo ambacho serikali haiwezi kuvumilia.

"Sisi tutawaonyesha hadharani ili wajulikane na hata wakienda mahakamani wakafanya michezo yao kumaliza kesi, jamii itakuwa imewafahamu na hii itasaidia watu wawaogope kama wabakaji," alisema.

Aidha alisema mtuhumiwa huyo alimrubuni mwanafunzi huyo amsaidie kupukuchua mahindi debe moja na akampa 'sado' moja kama ujira wa kazi. Alidai baada ya kazi hiyo alimvutia ndani na kumbaka.

Akizungumza mbele ya wanahabari, mkuu wa wilaya na polisi, Nnko alisema yeye si mhusika wa mimba hiyo. Alidai kuwa amesingiziwa na mwanafunzi huyo ambaye ni ndugu yake kwa sababu baba yake ni mdogo wake.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kikatiti, Amida Mnyenyelwa, alisema alipata taarifa shuleni kwa wanafunzi huyo kuhusu utoro wake na walianza kumfuatilia na wakabaini mjamzito.

"Tulipobaini tulimbana akamtaja huyu mzee Nnko kuhusika na alifanya naye tendo la ndoa mara mbili na hadi kumpa mimba hiyo," alisema.

Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Flora Nnko, alisema mtuhumiwa ni shemeji yake na alikuwa akimtuma mtoto wake kwenda kwa mtuhumiwa huyo kuchuma mchicha na kupukuchua mahindi bila hofu.

"Sasa tukawa tunashangaa kuona mtoto wetu anaumwa na mume wangu alipokwenda kumpima tukabaini mjamzito wa wiki nane na tulipombana na walimu wake akamtaja huyu shemeji yangu," alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo hana mke na anaishi mwenyewe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad