Baraka The Prince awavimbia wasanii "Sishei kitu cha mtu kwenye page yangu'


Msanii Baraka The Prince amesema kuwa yeye hawezi kukaa kutegemea msanii mwenzie amposti kwenye page yake huku akiweka wazi kuwa hashei kitu cha  msanii kwenye pegi yake.

Baraka amesema kuwa ukitegemea sana Support unafeli na hasa ukitegemea wasanii kwasababu akisema wao kama wana suppotiana ni unafki.

"Sitakaa nikaitaji page ya artist kwasababu still ye wale mashabiki wake, mimi sishare kitu cha mtu kwenye page yangu kabisa na ukiona nimepost mtu jua kaniomba sana na mimi nikishare kitu chako other wise nimekipenda sana," amesema Baraka.

"Ukitegemea sana support watu tunafeli sana kwa kutegemea support , tusidanganyane kwamba maartist wote tunasupotiana huo ni unafki tunaionyesha jamii ile kwamba tunasapotiana lakini real na kwenye moyo kabisa hakuna kabisa mtu kabisa eti anamsapoti mtu kiroho safi na ndio maana mimi huwaga na tabia moja siwei kuanza kukwambia kuwa nimekutumia kitu siwezi kukupigia kwamba we ushee inafaa wewe kusuport utapost," amesema Baracka kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad