Baraza la Mawaziri Uingereza Laidhinisha Rasimu ya Makubaliano ya Kujitoa EU

Baraza la Mawaziri Uingereza Laidhinisha Rasimu ya Makubaliano ya Kujitoa EU
Baraza la Mawaziri nchini Uingereza hatimaye limeidhinisha rasimu ya mswada wa makubaliano juu ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano makali yaliyoduymu kwa takriban saa tano,

Bi May amesema kwamba atawasilisha taarifa hiyo leo katika bunge la nchi hiyo, ambapo ataelezea uamuzi wa serikali.

Amekuwa mbioni kutetea mapendekezo ya mkataba baina ya Uingereza na muungano wa ulaya unaohusu masharti ya jinsi Uingereza itakavyoweza kujiondoa katika muungano huo.

Wafuasi wenye msimamo mkali wanaounga mkono Uingereza kujitoa kwenye muungano huo wanadai kuwa mkataba huo ni sawa na kusalimu amri.

Wamekuwa wakitoa wito wa kura kupigwa tena ili kuamua kama Uingereze ijitoe au kusalia kwenye muungano huo.

May pia amesisitiza bungeni kuwa Uingereza itajitoa kwenye muungano wa Ulaya.

"tuko katika hatua ya mgawanyiko" lakini mchakato wa Brexit,unaendelea na utatoa nafasi ya makubaliano hayo kukamilishwa.

Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya Brexit Michel Barnier amesema mswada huo wa makubaliano umewasilisha hatua ya maamuzi katika majadiliano, lakini bado kuna kazi ya kufanya.

Lakini Jacob Rees-Mogg mmoja wa viongozi wakuu wanaotaka Uingereza kujiondo kwenye muungano wa EU ameutaja mswada huo kama "mkataba uliyooza".

Mhariri wa BBC wa siasa za Uingereza Laura Kuenssberg amesema ni wazi kuwa baraza la mawaziri ''halikuzungumza kwa kauli moja'' huku mawaziri tisa wakiupinga mkataba huo wazi wazi .

Amesema kuwa ''naamini kuwa mvutano huu ni kwa maslahi ya Uingereza yote", akiongeza kuwa : "Ukiondoa pingapiza utaona wazi suala muhimu lililopo mbele yetu.''

"Mkataba huu unalenga kufanikisha uamuzi uliyofikiwa katika kura ya maoni, ambayo unarudisha usimamizi wa fedha zetu, sheria na mipaka, kukomesha uhuru wa utangamano, kulinda ajira, usalama na umoja wetu; au tuondoke bila makubaliano ama tusiondoke kabisa."

Yaliyomo kwenye rasimu hiyo ya makubaliano ya Uingereza kujitoa katika EU yamechapishwa pamoja na muongozo unaelezea kwa kina uhusiano wa Unchi hiyo na muungano wa ulaya utakavyokua siku zijazo.\

Inajumuisha kujitolea kwa Uingereza kulinda haki ya raia wa mataifa wanachama wa EU pamoja naraia wa Uingereza wanaoishi EU kuendelea kuendelea kuishi, kufanya kazi na kusoma bila hofu.
Kuna muda wa miezi 21 ya mpito utakaotolewa baada ya Uingereza kujitoa EU mwezi Machi mwaka 2019 na unajumuisha makubaliano ya kifedha kutoka Uingereza .

Suala lenye utata mkubwa katika mashauriano ya Brexit ni "uwajibikaji", linalo lenga kuhakikisha hakuna vikwazo vipya vya mpaka vinawekwa katika mpaka wa Uingereza na Ireland ikiwa taifa hilo halitakubaliana na makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya.
Pande zote mbili zimekubaliana kuwajibikia makubaliano mengine mbadala.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad