Benki Kuu Tanzania yataja maeneo ya kubadilishia fedha Arusha


Benki Kuu ya Tanzania imewataka wakazi wa Jiji la Arusha kuanza kutumia huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwenye maeneo ambayo yanatambulika kisheria ambayo yameainishwa kwenye taratibu za benki kuu.

 

Taarifa ya BOT iliyotolewa leo imesema kuwa “huduma za kubadilisha fedha za kigeni jijini Arusha zinapatikana kwenye hoteli za kitalii na benki za biashara kwa mujibu wa sheria na kanuni  za Benki Kuu ya Tanzania”


Aidha, huduma hiyo pia inapatikana nchini kote katika benki za biashara, maduka ya kubadilisha fedha na hoteli za kitalii.


Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa ghafla katika maduka ya kubadilisha fedha jijini Arusha tarehe 19 Novemba 2018 na kuamua Kuyafunga maduka yasiyozingatia taratibu na sheria za biashara hiyo.


Aidha BOT imewataka wakazi wa Jiji la Arusha kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho huduma za kubadilishia fedha zikiwa zimesitishwa kwenye maduka maalum.


“Benki Kuu inawashukuru wananchi wa jiji la Arusha kwa ushirikiano na kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.” imeeleza taarifa hiyo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad