Benki Kuu ya Tanzania Yatangaza kuongeza muda siku sitini (60) wa usimamizi wa Bank M PLC.

Benki Kuu ya Tanzania Yatangaza kuongeza muda siku sitini (60) wa usimamizi wa Bank M PLC.
Benki Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa usimamizi wa Bank M Tanzania Plc (Bank M) kwa siku 60 zaidi kuanzia tarehe 2 Novemba 2018.

Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu namba 56 (1) (g) (iii) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania ilichukua usimamizi wa Bank M kuanzia tarehe 2 Agosti 2018 baada ya kubaini kuwa benki hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

Baada ya kuchukua usimamizi, Benki Kuu ya Tanzania ilisitisha shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za Bank M kwa muda wa siku tisini (90) ili kuipa nafasi Benki Kuu ya Tanzania kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M haujakamilika; hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku 60 kuanzia tarehe 2 Novemba 2018,” kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad