Imefuta mkopo wa zaidi ya Tsh. Bilioni 700 uliokuwa utolewe kwa Tanzania kusaidia masuala ya elimu kufuatia wasiwasi uliopo kwenye sera ya kuwazuia Wanafunzi Wajawazito kwenda shule
Awali, benki hiyo ilizuia mkopo huo na kusema inafanya majadiliano na Serikali ya Tanzania na kuwa itaurejesha kulingana na makubaliano yatakayofikiwa
Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN, mkopo huo uliokuwa uidhinishwe na Uongozi wa benki mwishoni mwa mwezi uliopita lakini kwa sasa mpango huo umefutwa na hautaendelea tena
Aidha, hakuna takwimu rasmi za Wanafunzi wangapi Wajawazito wamekuwa wakiondolewa shuleni lakini kwa mujibu wa Kituo cha Haki za Kuzaliana cha Marekani mwaka 2013 kilisema kuwa takribani Wanafunzi Wajawazito 8,000 wamekuwa wakifukuzwa au kuondolewa shuleni kila mwaka