Billnass afunguka kumvimbia Nandy kwenye uzinduzi wa albam 'sikujiandaa kwa hilo'


Baada ya  msanii Billnass kumchunia Nandy wakati anajaribu kuimba nae katika kutambulisha album yake ya Africa Princes Billnass anasema hakuwa tayari kuimba na  sio kila sehemu anayoenda ashiriki kama msanii. 

Akiongea na E-NEWZ Billnass amesema kuwa alipopewa Mic na msanii huyo hakujua afanye nini huku akisema kuwa kuhudhuria tu katika uzinduzi huo ni support tosha. 

"Meza zote alipita anaimba na sikujiandaa kwa hilo tena nilikuwa nazungumza na mtu mwingine then nikakuta nakutana tu na Mic sikuwa najua nifanye nini kwahiyo ilikuwa hivyo kuhudhuria ni support tosha tulinunua Albam ni vitu ambavyo vinatosha kwa support," amesema Nandy. 

"Kwahiyo mi huwa na support pale ninapoweza hivyo , mi nilienda kuinjoy tu nakusikiliza muziki mzuri, mi nilikuja kama mhudhuria mwingine sio kila sehemu naenda kama msanii." 

November 9, 2018 ambayo ni siku ya kuzaliwa msanii huyo alizindua album yake ya 'Africa Princes'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad