Baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa jana, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi kupitia TFF, Boniface Wambura, amesema hakutakuwa na siku za nyongeza juu ya usajili wa wachezaji.
Wambura ameeleza hayo kutokana na utamaduni wa timu za kitanzania kuchelewa kufanya usajili wa wachezaji wakiamini kutakuwa na siku za nyongeza hapo baadaye.
Mkurugenzi huyo amesema katika mfumo huu mpya unaotumika kwa sasa maarufu kama TFF FIFA CONNECT hauna cha kuongeza muda hivyo kwa timu ambazo zinategemea ofa hiyo zisahau.
Dirisha limefunguliwa jana Novemba 15 ambapo litadumi mpaka Disemba 15 2018 wakati huo mechi za ligi zikiwa zinaendelea kama kawaida.
Tayari klabu kadhaa zimeshaanza kupigania saini za wachezaji wapya ili kujaza mapungufu ambayo yanazikumba timu zao.