CHADEMA Walaan Dereva wa Freeman Mbowe Kushikiliwa Polisi

k

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia hatua ya  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia kwa siku mbili  mtumishi wao Williard Urassa.


Urassa ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Novemba 24, 2018 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza tangu Urassa alipokamatwa na polisi, jeshi hilo limekataa kumpatia dhamana huku likizuia mtu yeyote kuonana naye.


Makene amesema zuio hilo limewakumba hadi wanasheria waliofika kwa ajili ya kumpatia msaada wa kisheria.


“Hali ambayo inaibua maswali mengi na sintofahamu kubwa kuhusu hali yake baada ya kukamatwa.


"Tunalaani na kukemea vikali kitendo hicho cha Jeshi la Polisi ambacho ni mwendelezo wa tabia inayopaswa kuachwa mara moja ya jeshi hilo kujipatia mamlaka lisilokuwa nayo, hasa kuwakamata na kuwashikilia chini ya ulinzi kinyume cha sheria,”imeeleza taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imesisitiza ni vyema jeshi hilo likatambua kuwa halina mamlaka ya kumshikilia mtu yeyote kwa namna hiyo.


Kulingana na taarifa hiyo Chadema imelitaka jeshi la polisi kueleza sababu za  kumshikilia dereva huyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad