CHADEMA Watoa Tamko Zito Baada ya Freeman Mbowe Kupelekwa Gerezani



Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimewataka wanachama wake nchi nzima kufika mahakamani wakati kesi inayowakabili viongozi wake watano itakapounguruma ili wajionee uendeshwaji wa kesi na kuamua kwa pamaoja nini cha kufanya.

Wito huo wa CHADEMA umekuja saa chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kuamua kufuta dhamana ya viongozi wawili wa chama hicho, Mwenyekiti wa chama taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini, Ester Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Akizungumza na wanahabari, makao makuu ya chama hicho yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji amesema, "wanachama wa CHADEMA nchi nzima, suala hili ni zito, ni nyeti na linahusu mustakabali wa nchi yetu, usisubiri kusimuliwa njoo uone mwenyewe kinachoendelea mahakamani kwasababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa".

"Tunaomba tuje tusikilize wenyewe mahakamani na baada ya hapo tuamue ni hatua gani tutachukua sisi kama watetea haki wa watu wote katika taifa hili," ameongeza.

Aidha katika hatua nyingine, chama hicho kimeazimia kukata rufaa katika Mahakama Kuu kwa kile ilichokidai ni kupinga juu ya hatua ya kufuta dhamana ya viongozi wake iliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

"Tumeamua kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu na tumeshawasilisha barua yetu, bado tunasubiria watupe namna. Na katika barua yetu tumeeleza haya mashaka yetu yote juu ya mwenendo wa hii kesi
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo nyie kina Mashinji mnafikiri huu Uhamasishaji wenu wa Chuki na Vuguvugu ya Kutaka kutuharibia amani yetu sisi wananchi tutakusikilizeni...
    Angalia huyu Mtowe wenu alipohamasisha Vurugu alikwenda nje kwa wanae.
    Wewe Mashinji familia yakoiko hapa hapa .. wenzako wamezitoa nje.

    Hii sakozi yenu ya Fujo na Mikusanyiko isiyokuwa na izini imesababisha Akwilina kututoka na wazazi wake ndiyo walioumia zaidi... na wataendelea kuumia mpaka haki ipite na wasababishaji wake wachukuliwe hatua stahiki....
    Msianze kujihami na kutufanya sisi kuwa waamuzi.. kwani hatukosomea uamuzi wa mitaani.

    Bebeni msalaba wenu wenye mlioutengeneza na ni lazima mheshimu mihimili yatu ya sheria .. Ukitaka kuona Dharau zenu zaidi... ni kwamba hapo hapo mjengoni kauli tata alizitoa Mtowe bila kuheshimu jengo la sheria alilokuwepo... na kutaka mapambano ... Ni UCHCHEZI MTUPPUUUUUU.....

    kUWENI WATU NA MJIHESHIMU ILI MIHESHIMIKE NA MIHEMUKO YENU MUIWACHE .

    h
    Hakuna atakae kuja.. Ajili tunawajua na Tumewachoka WACHOCHEZI NYIE.

    SAKOZI IMECHOKA NA POSHO ITAKOSA MGAWAJI SAFARI HII...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad