Chadema Yamjibu Makonda Kuhusu Kotoshiriki Kwenye Shughuli za Maendeleo

Chadema Yamjibu Makonda Kuhusu Kotoshiriki Kwenye Shughuli za Maendeleo
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetetea sababu ya wabunge wake kutoonekana kwenye baadhi ya shughuli za Maendeleo kwa kile walichokidai kuwa wabunge wake hawakupewa mialiko na wengine wakiwa na kesi mbalimbali mahakamani.

Majibu hayo ya CHADEMA yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusema kuwa wabunge wa upinzani hawaonekani kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumza na www.eatv.tv Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema “Makonda anasahau sana kuwa wabunge wetu walifukuzwa kwenye ofisi zao kinondoni, sasa atuambie hiyo mialiko huwa anaipeleka wapi.”

Akizungumza kwenye uzinduzi wa maktaba leo Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Paul Makonda amesema “nashangaa hata wale wabunge wapinzani wa Dar es salaam ambao mara nyingi wanakuja vyuoni kuwarubuni wanafunzi wawapigie kura lakini hawatokei kwenye shughuli za maendeleo, kazi yao ni kukosoa tu",

Aidha amesema kuwa wamekuwa wakijionesha kuwa ni wapiganiaji wa maendeleo kwa maneno na sio vitendo, huku akimpongeza Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa kwakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono wa shuguli mbalimbali za maendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad