Chama Cha CUF chamkana Zitto Kabwe

CChama Cha CUF chamkana Zitto Kabwe
Chama Wananchi CUF upande wa Profesa Lipumba umesema haufahamu chochote juu ya kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Selemani Bungala, na viongozi wengine.



Taarifa ya kukamatwa kwa viongozi hao zilianza kusambaa jana kupitia mitandao ya kijamii ambapo zilianzia kwa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye aliandika “nimezungumza na Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara akiwa kituo cha Polisi Kilwa, pamoja na Mbarara Maharagande, Msemaji wa Chama cha Wananchi ( CUF ) wamekamatwa na polisi na wapo kituoni kwa uchochezi”

Akizungumza na www.eatv.tv Msemaji Afisa Habari wa Chama  Cha Wananchi CUF ambaye ni Mkurugenzi wa Habari upande unaomuunga mkono Prof, Lipumba,  Abdul Kambaya amesema hafahamu chochote kuhusu suala la Mbunge wao kukamatwa na kutaka suala hilo atafutwe Zitto Kabwe aweze kulizungumzia.

“Sina taarifa ya kukamatwa, na kama ilisambaa mtandaoni basi ni mitandaoni siyo CUF, Zitto Kabwe siyo kiongozi wa CUF, hawezi kusema mambo ya CUF mimi sijibu taarifa za Zito Kabwe, muulizeni Zitto Kabwe athibitishe kukamatwa kwao.”

Chama Cha Wananchi CUF kimekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu wa kiuongozi juu ya pande mbili ikiwemo upande wa Profesa Lipumba, na Maalim Seif ambapo kila mmoja akidai mwenzake hana mamlaka kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

walipotafutwa viongozi wa CUF ambao wanamuunga mkono Maalim Seif ili kuzungumzia kukamatwa kwa viongozi hao hawakupatikana huku ikiendelea na jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Kilwa kuzungumzia tukio hilo nazo ziligonga mwamba.

Wakati wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale Mbunge, Suleiman Bungara “Bwege” aliwahi kusema, “ni jambo jema kwetu, tumeamua kuweka tofauti zetu pembeni, mimi nafanya kampeni japo simkubali Profesa Lipumba, huwezi kusema Nguruwe haramu halafu mchuzi wake si haramu kwa hiyo msimamo wetu tumeamua kuweka tofauti zetu pembeni kumuunga mkono Mgombea wetu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad