Chirwa Afunguka Baada ya Kusajiliwa ‘'Azam Wasipo Nipa Changu Navunja Mkataba''

Chirwa Afunguka Baada ya Kusajiliwa ‘'Azam Wasipo Nipa Changu Navunja Mkataba''
Klabu ya Azam FC imekubali kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na mchezaji wa zamani wa Yanga, Obrey Cholla Chirwa kwa mkataba wa mwaka mmoja.



Wakati akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari, Chirwa amesema kuwa wachezaji wengi wa Tanzania hawana msimamo huku akimwagia sifa Samatta kuwa amefanikiwa kutokana na msimamo wake hivyo hatoweza kuvumilia endapo atakosa haki zake ndani ya klabu.

”Wachezaji wa Tanzania hawana msimamo, mfano Samatta yeye anamsimamo hivyo na mimi ninamsimamo wangu kama mtu hanipi kitu changu ninachostahili navunja mkataba hapo hapo,” amesema Chirwa.

Obrey Cholla Chirwa ameongeza ”Hata Azam wasipo nipa naweza kuvunja mkataba nitasubiri nini naweza kuvunja kwasababu nina familia na inanitegemea hata wewe mwandishi familia inakutegemea unafanya kazi,” amesema hayo alipoulizwa na mwandishi wa habari.

”Kwa hiyo kama klabu inashindwa kunilipa kutokana na makubaliano yetu, naomba mikataba yangu niondoke kuna timu inanitaka Misri nimekataa timu Simon Msuva inanitaka, Supersport South inanitaka lakini maamuzi yangu ni bora nibaki hapa Azam FC ninajua tena nitatoka tena timu nyingine siwezi kuzitaja.”

”Azam ni timu nzuri kilakitu Azam FC kipo safi ndiyomaana nimeamua kukataa kwenda Moroco kwa SimonMsuva lakini kwa sasa malengo yangu ni kwenda kucheza mpira barani Ulaya kwa uwezo wangu nitafanikiwa kwenda.”

Chirwa amejiunga na Azam kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Nogoom El Mostkabl FC ya Misri baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa stahiki zake za kimkataba.
Klabu ya Azam inatarajia kumtangaza kama mchezaji wao kuanzia November 15 baada ya dirisha dogo la Usajili kufunguliwa. Chirwa aliomba kujiunga na Yanga SC ila kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera alimkataa kwa kusema hana uvumilivu timu ikiwa kwenye matatizo. Ndipo kocha wa Azam, Hans Van Der Pluijm akapeleka jina lake kwenye bodi ya Azam FC ili asajiliwe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad