CIA Wafichua Siri: Kiongozi wa Saudi Arabia Aliamuru Mauaji ya Mwandishi Khashoggi


Hitimisho hilo la CIA kuwa Mtoto wa Kifalme, Mohammed bin Salman aliagiza mauaji ya Mwanahabari, Jamal Khashoggi nchini Uturuki lina kinzana na taarifa ya Saudi inayodai hakuhusika

CIA imesema timu ya watu 15 ilienda Istanbul kwa kutumia ndege ya Serikali mwezi Oktoba na kumuua Khashoggi ndani ya Ubalozi wao alikoenda kuchukua nyaraka muhimu kwa ajili ya harusi yake na Mwanamke wa Kituruki

Ili kufikia hitimisho hilo CIA imedai kuangalia vyanzo mbalimbali vya taarifa ikiwemo kuingilia simu kati ya Balozi wa Saudi nchini Marekani ambaye ni Kaka wa Mohammed bin Salman, Khalid bin Salman na Khashoggi

Imeeleza Khalid alimwambia Khashoggi aende kwenye ubalozi wao huko Istanbul kuchukua nyaraka hizo huku akimuhakikishia kuwa ni salama kufanya hivyo
-
Haiko wazi kama Khalid alikuwa anajua kama Khashoggi atauawa ila baada ya kuongea na Mwanahabari huyo alipiga simu ambayo uelekeo wake ni aliko kaka yake, Kiongozi wa Saudi Arabia

Hata hivyo, Msemaji wa Balozi ya Saudi iliyopo Washngton, Fatimah Baeshen amesema Balozi wake na Khashoggi hawakuzungumza chochote kuhusiana na kwenda Ubalozi wao wa Istanbul na kusema taarifa ya CIA ni uongo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad