CHAMA cha Mwananchi (CUF) upande wa mwenyekiti wa chama hicho anayetembulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahimu Lipumba, wameibuka na kupinga vikali madai yaliyotolewa na aliyekuwa Mbunge wa chama hicho Jimbo la Temeke, Abdallah Mtolea, kuwa amekihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mipinduzi (CCM) ni kutokana na migogoro iliyopo ndani chama hicho, kikisema madai hayo siyo ya kweli.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Jafari Mneke, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini.
Mneke amesema madai aliyotoa mbunge huyo si ya ukweli bali chama hicho kinaamini kuwa Mtolea amejiuzulu kitokana kufuata vyeo ndani ya serikali kama walivyopata baadhi ya viongozi waliojiuzulu kipindi cha nyuma.
Akifanua baadhi ya hoja ikiweno suala la kumfukuza mbunge huyo, Mneke amesema chama hicho kilikuwa hakina hata mpango wa kumfukuza, kama kingekuwa na nia ya kumfukuza kingemfukuza tangu awali na wala hakukuwa na kikao chochote cha kumfukuza uanachama.
Kambaya amebainisha kuwa hata hoja anayodai kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho unamfanya mbunge kukosa ushikiano kwenye jimbo, Mneke amesema kukosa ushirikiano si kweli kwani mbunge akishachaguliwa na kuapishwa anapaswa kuwatumikia wananchi wake.
Katika hatua nyingine Chama hicho kimeipongeza serikali kwa hatua yake ya kununua mazao ya korosho ya wakulima huku kikisema hatua hiyo ina lengo la kumwinua mkulima .
Akitoa pongezi hizo kwa serikali, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa (CUF), Abdul Kambaya, amesema kwa kipindi kirefu chama hicho kimekuwa kikimlilia mkulima wa korosho kwa kuibiwa na baadhi ya wafanyabiashara, hivyo kitendo cha serikali ya Rais John Magufuli kununua korosho hizo kwa bei elekezi ya Sh.3,300 (elfu tatu na mia tatu) ni cha kupongezwa.
Hata hivyo, Kambaya ametoa wito kwa serikali kutazama changamoto zinazojitokeza kwa wakulima wengine wa mazao mengine ili kufanya utatuzi kwa wakulima wote.