Daimond Kuwashusha Mademu Wake Watano Mtwara Wasafi Festival

Daimond Kuwashusha Mademu Wake Watano  Mtwara Wasafi Festival
MADEMU ambao walishawahi kutoka kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wanatarajia kukutana kwenye tamasha kubwa la Wasafi linalotarajiwa kufanyika Mtwara, Novemba 24, mwaka huu. 



Taarifa zinaeleza kuwa, wanawake hao; Wema Sepetu, Kajala Masanja, Jacqueline Wolper, Anastazia Kimaro ‘Tunda’ na Irene Hilary ‘Lynn’ kila mmoja kwa wakati wake amealikwa kulipamba tamasha hilo litakalofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona na amekubali kuwepo.


“Kule hakuna cha aliyekuwa mpenzi wa zamani au wa sasa, sijui itakuwaje maana si unajua tena hisia za mapenzi huenda wakaanza kuleteana za kuleta au zile za kubinuliana midomo, tusikilizie,” alisema mtoa taarifa kutoka Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB).


Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, mbali na wanawake hao ambao walitoka na Diamond kwa nyakati tofauti, atakuwepo pia Lilian Kessy ‘Kim Nana’ ambaye ndiye anayeshikilia usukani wa penzi la Diamond kwa sasa.



“Diamond anataka kila mmoja asikose tamasha hilo kwa kuwa anaamini kuwa tamasha hilo ni kubwa na la kuleta mapinduzi ya burudani nchini,” alisema mtoa taarifa huyo huku Meneja wa WCB, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ akithibitisha uwepo wa warembo hao na wengine kibao kutoka Dar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad