DC Muro Azisaka Milion 400


DC MURO AZISAKA MILIONI 400

Na Imma Msumba, Arumeru
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Arumeru linamsaka aliyekuwa mweka hazina ( Muhasibu ) wa halmashauri ya meru Ndg. Emmanueli Joram na Michael Palanjo aliyekuwa mhudumu wa kawaida akapewa kazi ya wakala wa kukusanya mapato ya halmashauri kwa tuhuma za ubadhilifu wa ya shilingi Milioni 364 Fedha Za Miradi ya TASAF kwa halmashauri ya Meru, uku Shilingi milioni 119,674,285 zikiwa pia hazionekani katika akaunti ya halmashauri ya Meru zikiwa ni fedha za makusanyo ya ndani ambazo hazijapelekwa benki na hazijulikani zilipo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Halmashauri hiyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. JERRY MURO ambapo amefanya ziara yake ya kushtukiza katika Halmashauri hiyo na kubaini kiasi hicho cha fedha kupotea na ameshangazwa na upotevu huo kuchukua muda mrefu bila uchunguzi.

Kwa upande wake msimamizi wa mfuko wa Tasaf Ndg. Bonifasi Mwilanga mbali na kukiri kufahamu kwa ubatilifu huo amekiri pesa hizo zimetumika kinyume cha utaratibu katika matumizi yake.

Pia kwa upande wao baadhi ya viongozi wa Halmashauri hiyo akiwemo Mkurugenzi Ndg. Emmanueli Mkongo na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ndg. Wille Njau wamelezea jitihada walizozichukua ikiwa ni pamoja na kuunda kwa tume ya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha hizo.

Dc Muro amewaagiza wakuu wa idara zote katika Halmashauri hiyo kutosubiri taarifa za fedha za idara zao na badala yake ni kufatilia kila Juma kimaandishi ili kutotoa mwanya wa upotevu wa pesa za umma.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad