Denmark Yasitisha Msaada Tanzania Kutokana na Kauli Dhidi ya Wapenzi wa Jinsia Moja

Denmark Yasitisha Msaada Tanzania Kutokana na Kauli Dhidi ya Wapenzi wa Jinsia Moja
Nchi ya Denmark imezuia krone milioni 65 ($9.8 milioni) ambazo zilikuwa ni msaada kwa Tanzania baada ya kutolewa "kauli zisizokubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja" kutoka kwa mwanasiasa mwandamizi.

Hatua hiyo ya Denmark imetangazwa na waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo Ulla Tornaes. Bi Tornaes hata hivyo hakumtaja kwa jina mwanasiasa mwandamizi wa Tanzania aliyetoa kauli hiyo ambayo wanasema haikubaliki na kushtusha.

Mwezi uliopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitangaza operesheni dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kwa kutaka watu wawaripoti polisi watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Makonda pia alitangaza kamati maalum ambayo pamoja na shughuli nyengine ingeliangazia suala hilo la wapenzi wa jinsia moja.

Serikali hata hivyo ilijitenga na kauli hiyo ya Makonda kwa kudai alikuwa akitoa mtazamo wake na si sera rasmi ya nchi.

Kufanya ngono kinyume cha maumbile ni kosa la jinai nchini Tanzania na mtu akipatikana na hatia anaweza kuadhibiwa kifungo cha miaka 30 ama maisha jela. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na kukazwa kamba dhidi ya watu wanaojihusisha na matendo hayo.

Mwaka 2017, aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya alitetea tishio la kutaja listi ya wapenzi wa jinsia moja.

Nimeshtushwa na mambo hasi yanayoendelea Tanzania. Hivi karibuni ni kauli imetolewa kauli isiyokubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kamishna," ameandika Bi Tornaes kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

"Kutokana na hilo nimezuia msaada wa DKK 65m kuelekea nchi hiyo. Kuheshimu haki za binaadamu ni jambo kubwa kwa Denmark."

Denmark ni nchi ya pili kwa kutoa misaada kwa Tanzania.

Waziri huyo pia amesitisha ziara yake nchini Tanzania, shirika la habari la nchi hiyo DR limeripoti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad