Diamond Azindua Rasmi Wasafi Festival na Wasafi FM...Clouds FM Wanalo


Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB) leo imezindua kituo cha redio cha Wasafi FM pamoja na tamasha la Wasafi litakalofanyika katika maeneo mbalimbali nchini. 

Mkurugenzi wa WCB, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' amesema uzinduzi wa redio hiyo unalenga kutoa fursa kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla kusikika. 

"Siku ya leo redio yetu ya Wasafi FM itaanza kusikika kupitia masafa ya 88.9 katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Bado ndio tupo kwenye majaribio kwani mambo mazuri yanakuja na tumefanya hivi kwa sababu hata sisi wenyewe tulifanikiwa kwa sababu tulisapotiwa na vyombo vya habari," alisema Diamond. 

Kuhusu Tamasha la Wasafi, Diamond alisema mbali ya kuburudisha, watafanya huduma za kijamii na kutangaza utalii. 

"Licha kufanya tamasha, sisi tungependa kuonyesha kitu cha tofauti. Tutajitahidi katika kila mkoa tunaoenda kurudisha kwa jamii kile ambacho tunakipata kutoka kwao. Tutaangalia changamoto ya eneo husika kama itakuwa ni elimu basi tutatoa sare za shule, madawati na kadhalika. Pia tutatangaza utalii," alisema Diamond. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad