Dr Slaa Aitwa Kuhojiwa na Serikali ya Sweeden


Balozi huyo wa Tanzania nchini humo ameitwa ili ajieleze kuhusu kudorora kwa Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala wa Sheria katika utawala wa Serikali ya Awamu ya 5.

Wakati huo huo Mabalozi wengine wa Tanzania kwenye nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU) nao wameitwa kutoa maelezo

Aidha wameeleza kusikitishwa kwao na oparesheni dhidi ya Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Mataifa makubwa pamoja na Mashirika ya Kimataifa kwa nyakati tofauti yamekemea na kuishutumu Serikali ya Rais Magufuli kwa kuminya Haki za Kiraia, Uhuru wa Habari na Kujieleza, Haki za Binadamu na Demokrasia
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad