Emmanuel Mbasha 'Mchungaji Aliemuombea Rosa Muhando Amemdhalilisha na Kumfanya Adharaulike"


Kutoka kwa @e.mbasha

'Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.

Kwa unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.

Katika nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa, ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea. Rose Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.

Biblia inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani vile.

Hali hii inaweza kumtangaza sana muombeaji lakini kwa upande wa muombeaji inaweza kuzidisha tatizo na kusababisha adharaulike zaidi kwenye jamii inayomtazama. Watumishi wa Mungu mahitaji kuwa na hekima pamoja na kifua cha kutunza siri, na siyo kufanya mambo kwa mihemko huku mkitazama maslahi yenu.

Mimi nadhani ingekuwa bora sana endapo mchungaji angemuombea ofisini, na kama maombi yangeleta majibu naamini video ya shuhuda ambayo Rose Muhando ange ongea wakati akiwa na akili zake timamu ndiyo ingefaa kusambaa na kuendelea kumjengea heshima yeye pamoja na mtumishi aliyemuhudumia.

Kumbuka yule Akida (mkuu wa vikosi cha askari wa kirumi) alipohitaji maombi kwa Yesu, Biblia inasema Yesu alifunga safari kwenda nyumbani kwake ili kumuombea. Unadhani kwanini hakumwambia apelekwe amuombee hadharani kama alivyofanya kwa Batromayo? Hii ilikuwa ni hekima ya kulinda heshima ya muombewaji. Maana huwezi kumuombea Rais kama unavyoombea ombaomba au mpiga debe.

Kwa kweli nimeamua kuwa muwazi na kuziweka huzuni zangu hadharani ili waombeaji mjirekebishe. Siyo kila maombi yafanyike wakati caméra ziko on, kuna mengine ya kuzima camera na kuomba kwa staha ili kuendeleza uhai na kipawa'

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...I am with you Mbasha. Maombi na mahitaji ya watu ni siri yao na Mungu pqmoja na aliyeshirikishwa. Mwombaji huyu nahisi alitafutabkukuza jina lake lakini siyo kuendelea kujenga heshima na hadhi ya mtumishi mwenzake ambaye ni Rose. kwa ujumla nilisikitishwa na kitendo kile cha kuanika mtumishi wa Mungu aliyevamiwa hadharani na hii haimpi Mungu utujufu bali wengi huvunjwa moyo hasa waliokuwa nyuma ya Rose.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad