Fatma Karume Amtuhumu Uchawi Waziri Kigwangalla, Amjibu “Hujui kibuyu”


Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbao la Nzega Vijijini la Mkoani Tabora, Dkt. Hamisi Kigwangalla alifanyiwa tambiko la kichifu na Wazee wa Mila na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma ambapo walimtambikia ili akawe tayari kwa kazi za kulitumikia Taifa katika majukumu ya Kibunge na Uwaziri.

Tambiko alilofanyiwa Waziri Kingwangalla limezua mjadala Twitan ambapo watu wamelihusisha na imani na kishirikina, akiwemo Rais wa TLS Fatma Karume na wengine good thing ni kwamba Waziri alikuwa akijibu.

Alianza hivi Fatma Karume
 “Dkt wa medicine anaamini ujinga huu wakutisha watu kwa kutumia wachawi?. .”

Waziri Kigwangalla hakuacha ipite kimya akamjibu
“Shangazi, hizi makitu wewe hujabobea hivyo hata huelewi kama hii ni ndumba, tambiko ama ibada za jadi! Wewe siyo Mkimbu mwenzangu! Wala Mnyamwezi au Msukuma! Wala siyo Mtemi kama mimi! This thing is ‘Greek’ to you! Umekulia ikulu ukiona kibuyu unajua uchawi”

Nae Fatma akarudi tena kumjibu
“Nikiona UBUYU na ULA!!! Kwetu unapikwa kwa sukari na rangi nyekundu na pilipili kidogo. Hatuuabudu!!! Tunautafuna kwa raha zetu.”

Waziri Kigwangalla akajibu hivi
“Shangazi, si unaona sasa? Hata tofauti kati ya ‘UBUYU’ na ‘KIBUYU’ hujui! Wewe unaongelea ubuyu, chakula! Mi naongelea kibuyu, chombo kule kwetu. Unachemka halafu unatukana kwa kujiamini kabisa, kama mpumbavu, mwehu ama mlevi!”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad