Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga amesema kuna oparesheni maalum ya ukaguzi na udhibiti wa uendeshaji biashara ya fedha jijini Arusha.
Prof. Luoga amezungumza hayo baada ya askari wa JWTZ kuonekana wakiyalinda maduka ya kubadilishia fedha tangu jana asubuhi.
“Uchunguzi wa Benki Kuu umebaini kuongezeka biashara ya ubadilishaji na utakatishaji fedha. Kuna maduka hayajasajiliwa lakini yanafanya biashara hii kinyume cha utaratibu” -Prof. Luoga.
“Wote watakaobainika kukiuka sheria watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote waliokuwa wanaendesha maduka hayo bila kufuata utaratibu leseni zao zimesitishwa” Prof. Luoga
Gavana wa BOT Afunguka Kuhusu Wanajeshi Kulinda Sehemu za Kubadirisha Fedha za Kigeni
0
November 20, 2018
Tags