Harufu ya penzi la Diamond na Nandy ‘ilivyochafua’ hali



Diamond Platinumz ambaye amekuwa akijitangaza kuwa ni ‘bachela’ tangu aachane rasmi na mama watoto wake, Zari na Hamisa ametuliza moyo wake mikononi mwa Nandy?

Hilo ndilo swali tata lililotawala mitandao ya kijamii jana, baada ya Bosi huyo wa WCB kuweka mtandaoni vipande vya video vinavyowaonesha wawili hao wakiwa na ukaribu wa ‘mapenzi la njiwa’ ndani ya Dubai.

Video ya kwanza ambayo ilimuonesha ‘akicheza’ na kidevu cha Nandy kwa mbali, ilipigiwa mstari na video ya pili ambayo ilimuonesha akiwa na mrembo huyo aliyevalia cheni kubwa ya WCB, huku wakiwa na ukaribu usioacha nafasi.

Vipande vilivyofuata vilizidi kuchochea hisia ya harufu ya penzi kati ya wawili hao, ambapo moja ilimuonesha Nandy akiwa amekaa sehemu inayoaminika kuwa ni jiko, hali iliyojenga picha kuwa walikuwa wanashea nyumba moja.

Hata hivyo, Diamond alikoreza tetesi hizo kwa kipande kingine cha video inayoonesha wakiwa gizani, na kuandika ‘Watoto Mkalale’.


Video za awali pia zimeacha utata wa tafsiri ya uhusiano wa wao, ambapo alimtambulisha kwenye video moja kuwa ni ‘mama enu… bi mkubwa’. Majina hayo yote yana uhusiano na mwanamke ambaye unaukaribu naye usio wa kirafiki tu.

Harufu hiyo ya penzi jipya kati ya wakali hao wa Bongo Fleva imeongeza utata mwingi, hususan kutokana na kusadikika kuwa Diamond na timu ya WCB, wana uhasama na Ruge Mtahaba ambaye ni Bosi wa Nandy kwenye muziki.

Haijafahamika dhahiri kama Nandy atakuwa ni mmoja wa watakaotumbuiza Wasafi Festival au kuna zaidi ya kutumbuiza kwenye jukwaa hilo.

Nandy na Diamond walikutana Dubai walipoenda kushiriki tamasha kubwa la muziki Afrika, ambalo liliwahusisha pia wasanii kama Wizkid, Vanessa Mdee na wengine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad