Hatma ya Mbowe,Uenyekiti wa Lipumba kufahamika leo

Hatma ya Mbowe,Uenyekiti wa Lipumba kufahamika leo
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam hii leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi juu ya dhamana inayowakabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko.

Kesi hiyo iliyotajwa jana, ilishindwa kukamilika baada ya upande wa Jamhuri kupeleka pingamizi juu ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambapo Jaji wa Mahakama hiyo, aliamuru isikilizwe na kutolewa uamuzi leo.

Mbowe na Matiko wanakabiliwa na tuhuma za kushindwa kuhudhuria kesi yao inayowakabili pamoja na viongozi wengine wa chama hicho mara kwa mara, hali iliyopelekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuta dhamana yao kabla ya kukata rufaa Mahakama Kuu.

Kesi nyingine inayotarajiwa kutolewa uamuzi leo katika Mahakama Kuu ni kesi ya kikatiba ya Chama cha Wananchi CUF dhidi ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ambaye aliachana na chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 na kutangaza kurejea katika nafasi yake mwaka mmoja baadaye.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ni wanachama wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad