Almasi yenye rangi ya waridi huwa ni adimu kupatikana na gharimu yake ni dola milioni 50 kwa karati.
Almasi hiyo ambayo ni ghali na ina uzito wa chini ya karati 19.
Almasi la waridi ilinunuliwa na chapa ya Harry Winston mwenye asili ya Marekani katika mnada uliofanyika Geneva.
"Karati moja inagharimu takribani dola milioni 2.6 na bei hiyo inathibitisha kuwa almasi ya rangi ya waridi ina gharama kubwa zaidi duniani", kwa mujibu wa mkuu wa nyumba ya mnada barani ulaya, Christie.
Almasi hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya kati ya dola milioni 30 mpaka dola milioni 50 baada ya kuuzwa kwenye mnada ndani ya dakika tano.
Mmiliki mpya wa almasi ya waridi ameipa jina la Winston Pink Legacy.
"Mwanzoni almasi hiyo ilikuwa inamilikiwa na familia ya Oppenheimer ambayo ilikuwa inamiliki mgodi wa De Beers,
Unaweza kusema kwamba almasi yenye rangi ya waridi ina uzito wa karibu karati 19 .
Hii inashangaza," Rahul Kadakia kutoka duka la kimataifa la vito alieleza.
Na almasi hii inadaiwa kuwa ni ya kifahari na iko katika daraja la juu zaidi ya almasi nyingine.
Kipande hicho kilipatikana katika mgodi mmoja wa Afrika kusini takribani miaka mia moja iliyopita na inawezekana hakikuwahi kubadilika tangu mara ya kwanza ikatwe mwaka 1920,
Christe alibainisha.
Almasi ya kifahari ya waridi ambayo ina uzito mkubwa zaidi ya karati 10 iliuzwa katika mnada wa almasi ya waridi iliuzwa kwa duka la kimataifa vito.
Mwezi Novemba 2017,8.14 karati ya rangi ya waridi iliuzwa kwa dola 17,768,041 mjini Hong Kong na karati nyingine ziliuzwa dola milioni 2.1kwa karati.