Henry Mwaibambe, kamanda wa jeshi la polis kanda maalum Tarime Rorya akizungumza akiwa katika eneo la tukio ameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa bado hakijajulikana lakini dereva wote kwenye ajali hiyo wamepoteza maisha.
“Kuna watu wengine ambao hawajatambuliwa, tunajitahidi ili watambuliwe, chamsingi ambacho hakina ubishi madereva wote wamefariki, lakini tunaendelea na uchunguzi ili kujua idadi kamili ya watu waliofariki hatuwezi kuwaficha marehemu,” amesema Kamanda Mwaibambe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime Bw. Glorius luoga ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuwataka madreva kuwa makini pindi wanapokuwa wamebeba abiria kwenye vyombo