Idris Sultan Amuangukia Rais Magufuli ‘hii Nchi Inapoteza Wazalendo Siku hadi siku’

Idris Sultan amuangukia Rais Magufuli ‘hii nchi inapoteza wazalendo siku hadi siku’
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Idris Sultan amemuandikia barua ya wazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John P. Magufuli akielezea mtazamo wake juu ya madhara ya kufutwa kwa sherehe kubwa kama za Uhuru.


Idris kwenye barua hiyo fupi, aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii ameeleza kuwa, sherehe hizo zinafaida kubwa kwa vijana ikiwemo kujenga uzalendo na kujua historia ya taifa lao.

Dear Mheshimiwa Raisi,
I love you work ethics na jinsi ulivyo na uchu wa maendeleo ndio maana nilikusapoti 2015. Nasema hayo ili ujue I’m with you mostly na akupendae sio mnafki. Hii nchi inapoteza wazalendo siku hadi siku na siwezi laumu kwasababu watu wanakosa passion.

This is a beautiful country tena sana ila watu wake hatujui uzuri wa hii nchi na tuipende vipi. Kutengeneza uzalendo kuna umuhimu wa kuijua historia yetu kwa undani. Ili watu waweke attention kwenye historia basi muhimu kuonyesha uzito wa matendo yaliyofanyika katika historia.

Kuonyesha uzito huo basi ni kuadhimisha makubwa yote yaliyofanyika katika historia. Kama nilivyosema juu “Tunapoteza wazalendo” vijana wadogo sasaivi wanakua wakiichukulia nchi poa poa tu. Hawajui uzito wa uhuru walionao kutembea kwenye hii ardhi.

Vitu kama hospitali ni muhimu sana ila natamani ingekuwa kwenye bajeti yake ya afya. Isifike wakati tuchague kati ya kusherehekea juhudi za kutafuta uhuru wa nchi na afya. Kila sula lina umuhimu wake. Ni ngumu kuchagua either ule au upumue. We need both.

I’m scared we are losing patriotism na kidogo kidogo tutatengeneza vijana wanaopata madaraka katika ofisi yako ila wataangalia maslahi yao tu. Yes inafika huko. It’s too late umefanya maamuzi na you’re the president ndio kauli ya mwisho ila naomba ulione hili katika jicho langu

Wiki hii Rais Magufuli ametangaza kufuta sherehe za Uhuru zinafanyika kila mwaka mwezi Desemba 9, 2019.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad