Kajala "Nikipata Mwanaume Mkweli Naolewa Tena Mara ya Pili"
0
November 25, 2018
Mwanamama mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kudai kuwa akipata mwanaume mkweli, mwenye upendo ataolewa kwa mara ya pili. Kajala aliliambia Risasi Jumamosi kuwa yeye kama mwanamke bado anatamani kuingia kwenye ndoa na akitokea mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ataolewa kwa mara ya pili.
“Nilishaolewa mara ya kwanza, lakini kama mwanamke bado ninahitaji kuolewa, suala hilo lipo akilini kwangu, akitokea tu mwanaume mkweli, naolewa,” alisema Kajala. Kajala aliolewa ndoa ya kwanza na mumewe Faraji Chambo ambaye alitengana naye baada ya kupata matatizo yaliyosababisha wao kuhukumiwa kufungwa jela.
STORI:Imelda Mtema, Dar
Tags