Kala Jeremiah atembelea mahali ambapo alikuwa akiuza mitumba

Kala Jeremiah atembelea mahali ambapo alikuwa akiuza mitumba
Msanii wa muziki wa HipHop nchini, Kala Jeremiah ametembelea mahali ambako alikuwa akifanya kazi ya kuuza nguo za mitumba, kazi ambayo alikuwa akiifanya kabla ya kutoka kimuziki.

Kala Jeremiah ameitaja sehemu hiyo maarufu kama "Mlango mmoja" iliyopo jijini Mwanza kuwa ndipo mahali ambako alifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

 "Jana nilifanikiwa kuingia mlango mmoja au langolango sehemu niliyokuwa nikiuza mitumba jijini Mwanza, nimefurahi kuwaona rafiki zangu ambao nilifanya nao biashara kwa miaka 3 japo kuna wengi sikuwakuta kutokana na kuwa jana ililiwa jumapili. Nimesikitika sana kuona nusu ya soko limeungua na kusababisha hasara kubwa sana," amesema Kala alipofika eneo hilo.

"Nawaombea kwa mungu ndugu zangu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu. Pia naziomba mamlaka zinazohusika ziharakishe namna ya urudishiaji wa soko hili muhimu sana na lililoajiri vijana wengi sana na linategemewa sio Mwanza tu bali Kanda yote ya Ziwa," ameongeza.

Pia Kala Jeremiah ametumia nafasi ya kutembelea sehemu hiyo kwa kutoa historia fupi ya maisha yake wakati anauza mitumba, ambapo amesema,

"Soko hili ndilo lililosababisha leo mimi niko hapa, wakati naanza kufanya biashara ya mitumba 2002 sikuwa nashabikia sana HipHop nilikuwa shabiki wa bolingo na nyimbo za injili lakini nilipoingia humu nikakuta utamaduni wa humu ni HipHop na mimi nikaunga msafara mpaka 2004, sikuwa hata najua kuwa nina kipaji cha muziki ila kutokana na mapenzi  nikajikuta naanza kuchana (ni story ndefu) lakini pia nilipokuwa 'BSS' watu wa soko hili walikuwa wanapitisha daftari la mchango na pesa inayopatikana wananipigia kura muuza mtumba mwenzao. upendo huu hunifanya nione kuwa hawa ni ndugu zangu wa damu. Nawapenda sana."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad