Kampeni za Uchaguzi Zaanza DRC Hali ya Usalama sio Shwari

Kampeni za Uchaguzi Zaanza DRC Hali ya Usalama sio Shwari
Kampeni za uchaguzi wa urais zinaanza leo ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huku kukiwa na mpasuko mkubwa kwenye upande wa upinzani na hofu juu ya usalama.

Mwisho wa wiki iliyopita wafuasi watatu wa chama tawala cha rais Joseph Kabila wanaripotiwa kuchinjwa katika jimbo la Kasai walipokuwa wakifanya kampeni.

Kura ya kumchagua mrithi wa Kabila aliyekaa madarakani kwa mika 17 itafanyika tarehe 23 ya mwezi ujao, Desemba 2018.


Wiki iliyopita Martin Fayulu alichaguliwa kusimama kama mgombea kinara wa upinzani na ameungwa mkono na wapinzani wengine wenye ufuasi mkubwa kama Moise Katumbi na Jean Pierre Bemba.

Hata hivyo, chama cha upinzani chenye wafuasi wengi zaidi nchini humo cha Union for Democracy and Social Progress tayari kimejitenga na mgombea huyo. Chama hicho kinaongozwa na Felix Tshisekedi kimekuwa mstari wa mbele dhidi ya utawala wa kabila.

Martin Fayulu (kati) alichaguliwa kusimama kama mgombea kinara wa upinzani lakini tayari wapo waliojitokeza kumpinga
Kiongozi mwingine wa upinzani Vital Kamerhe pia alijitoa kwenye makubaliano hayo akisema hakukuwa na uungwaji mkono wa kutosha kutoka mashinani baina ya wanachama.

Je Emmanuel Ramazani Shadary, ni nani?

Endapo mgogoro huo ndani ya upinzani utaendelea kupamba moto itakuwa ahueni kwa mgombea kutoka chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary.

Shadary anaonekana na wengi kuwa ni kibaraka wa Kabila ambaye amezidisha muda wake madarakani kwa miaka miwili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad