Kampuni ya Fastjet Plc iliyoorodheshwa katika soko la hisa la London, Uingereza inatarajia kuuza hisa zake 49% katika Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania
Inaelezwa ni baada ya kujiendesha kwa hasara kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ushindani kutoka ATCL, changamoto za kisheria na uwezo wake wa kukusanya fedha
Aidha, inadaiwa kuondoka kwa Fastjet Plc kutaliacha shirika la Fastjet Tanzania na uwezo mdogo wa kushindana na mashirika mengine ya ndege
Shirika hilo limeeleza kukumbwa na changamoto cha kisheria ikiwemo kuchukua muda mrefu kwa ndege zake mpya 3 aina ya ATR72-600 kuruhusiwa kuanza kufanya kazi