Waitara ambaye ameteuliwa na Rais Magufuli katika nafasi hiyo hivi karibuni, amesema kama mkuu wa mkoa ameona kuna jambo la dharura na muhimu kama la elimu ana haki ya kuahirisha likizo hizo ili usimamizi uendelee na watakwenda baadae.
''Uzuri wa sheria za utumishi wa umma zinaruhusu likizo kusongezwa mbele kwahiyo mtumishi anaweza kuomba tu baadae akenda na kwa hili nadhani wakisimamia madarasa yakakamilika, watakaa na kuelewana lini waende likizo kwahiyo hilo halina shaka'', amesema.
Akiwa katika moja ya vikao vya utekelezaji wa miradi, Mh. Nchimbi alifuta likizo za baadhi ya watumishi akiwemo, yeye mwenyewe, Wakuu wa wilaya, RAS na wakuu wengine wa idara ili kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa Madarasa.
Waitara amesisitiza kuwa lazima watumishi wawe waelewa hususani kwenye jambo la msingi kama hilo, wala hawajaonewa na haki yao watapata ila hili la elimu ni kipaumbele kikubwa cha taifa.