Wakili wa serikali Mkuu, Vitalis Peter Leo Novemba 14, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka lakini hawapo tayari.
Kwa sababu wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo amepatwa na dharura na kwamba tatizo linalomkabili halijatatulika na hivyo wakili Peter aliiomba Mahakama waandae ushahidi mwingine ili waweze kuendelea naye.
Baada ya Wakili Peter kueleza hayo, Hakimu Simba alisema, “kwa mtindo huu hii kesi haitomalizika sasa hivi, tutakuwa tunacheza tu.
Hakimu Simba aliongeza, “sasa muwe mnaleta mashahidi wawili wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea na kwamba hali kama hiyo imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne ama tano.
Upande wa utetezi uliwakilishwa na mawakili Alex Mgongolwa, Semi Malimi, Nduluma Majembe, Denis Tumain na John Mhozya.
Kwa upande wake wakili Mgongolwa alitaka mashahidi wanaokwenda kutoa ushahidi katika kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta ana tatizo watafute mwingine.
Hakimu Simba alisisitiza upande wa mashtaka kupelekwa mahakamani hapo mashahidi wawili wawili na kuiahirisha kesi hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo wataendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.