Kuamka Mapema Kunaweza Kukuepusha na Gonjwa la Saratani

Wanawake wanaoamka mapema wapo katika uwezekano mdogo wa kupata saratani ya matiti, kwa mujibu wa watafiti nchini Uingereza. Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Briton wanasema sababu ya uhusiano wa muda wa kuamka na hatari ya saratani bado inahitaji kufahamika. Wanaongeza kuwa ugunduzi huo ni muhimu kwa kuwa unamuathiri mwanamke.

Kila mtu ana kile kinachofahamika kama saa ya mwili ambayo inaonyesha jinsi mwili unafanya kwa saa 24. Hi inajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama circadian rhythm. Inaathiri kila kitu kutokana na muda tunaolala, hisia zetu na hata hatari yetu ya kupatwa na mshituko wa moyo.

Lakini si kila saa ya mwili ya kila mtu inayoonyesha muda ulio sawa. Watu wa asubuhi au “larks” huamka mapema, hufanya kazi mapema na huchoka mapema. Watu wa jioni au “owls” huwa na wakati mgumu kuamka mapema, na hupenda kulala wakiwa wamechelewa.

Watafii wanafikia hivyo. Walitumia njia moja ya kuchambua data inayojulikana kama Mendelian randomisation. Walichunguza DNA inayoonyesha ikiwa sisi ni watu wa asubuhi au watu wa jioni. Walitumia taarifa hizo kuwafanyia majaribio wanawake 180,000 nchini Uingereza. Walionyesha kuwa watu walio na jenetiki za kurauka mapema walikuwa katika hatari ya chini ya kupatwa na saratani ya matiti kuliko wale walio na tabia za kutomka asubuhi.

Karibu mwanamke mmoja kati ya saba hupata saratani ya matiti nchini Uingereza katika maisha yake. Lakini uchunguzi huu uliangazia kiasi kidogo cha maisha ya mwanamke. Katika kipidi hicho ilibainika watu wawili katika  watu 100 wasiorauka mapema walipata saratani ya matiti ikilinganishwa na mmoja kati ya watu 100 waliomka mapema. Umri na historia ya familia ni baadhi ya masuala yanayochangia mtu kuwa na saratani.

Si rahisi namna hiyo. Dkt Richmond amesema bado ni mapema kuwapa ushauri wa moja kwa moja wanawake juu ya suala hilo. “Bado tunahitaji kujua kwa nini mtu anayechelewa kuamka kuwa yupo kwenye hatari kuliko wa asubuhi…Inabidi tufumbue fumbo hilo kwanza.” Bado kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu juu ya uhusiano wa kuwahi ama kuchelewa kuamka na uwezekano wa kupata saratani.

Je watafiti wapo sawa?
Sayansi kwa kawaida haitoi majibu ya uhakika kwa asilimia 100, lakini utafiti huu tayari una mashiko. Shirika la Afya Duniani (WHO) katika moja ya tafiti zao wameonesha kuwa kujinyima usingizi ama kuusumbua mwili kutoka usingizini mapema kuna uhusiano na hatari ya kupata saratani.

Dkt Richard Berks kutoka taasisi ya Breast Cancer Now, amesema: “Matokeo ya utafiti huu yanaongeza ushahidi uliokuwepo juu ya uhusiano wa usingizi na kansa ya matiti, lakini utafiti zaidi unahitajika ili kupata majibu ya baadhi ya maswali ambayo yanagonga vichwa.”

GPL
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad