Kufa na Kupona Alama 3 Kuipeleka Tanzania AFCON kesho
0
November 17, 2018
NA ELBOGAST MYALUKO
Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kufuzu fainali za AFCON 2019 nchini Cameroon, baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa 5 wa kundi L hivyo kufikisha alama 13 kwenye Kundi L.
Bao pekee la ushindi limefungwa na mshambuliaji Patrick Henry dakika ya 78 na kuwahakikishia Uganda kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu iliyopita wakifanya hivyo mwaka 2016.
Uganda sasa wamekuwa vinara wa kundi L wakifuatiwa na Tanzania ambayo ina alama 5 katika mechi 4 huku Cape Verde wakiwa na alama 4 katika mechi 5. Lesotho wanashika mkia wakiwa na alama 2.
Tanzania italazimika kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Lesotho ili ipate alama 3 na kufikisha alama 8 ambazo zitawafanya wafuzu moja kwa moja kutoka na Cape Verde kutokuwa na uwezo wa kuzifikia hata kama wakishinda mechi zao za mwisho.
Timu nyingine zilizofuzu ni wenyeji Cameroon, Madagascar, Nigeria, Senegal, Morocco, Misri na Tunisia.
Tags