Lema, Ndugai Wapambana tena

Lema, Ndugai Wapambana tena
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless amedai kuwa Bunge linaloongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai limepoteza mvuto kwa kile alichokidai kuwa maamuzi mengi hayafanywi na Bunge hilo huku akishindwa kueleza ni nani anayefanya maamuzi hayo.

Kwa mujibu Godbless Lema, morali wa kufanya kazi za kibunge unapungua na kuwalazimisha wabunge hao wa upinzani kuongeza nguvu zaidi nje ya bunge ili kuhakikisha wanawaondoa wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na www.eatv.tv Lema amesema “kwangu mimi bunge limepoteza hadhi sio maamuzi ya wabunge yanayoweza kusababisha mabadiliko ya taifa hili, kwa maana hiyo morali ya kufanya kazi ya kibunge ndani ya bunge inapungua na badala yake inatulazimu kujenga wigo mpana nje ya bunge, ili inapokuja uchaguzi wa  2020 tuwaondoe wabunge wa CCM.”

Naye Spika, Job Ndugai akizungumza juu ya madai hayo ya Lema, amesema  “hilo jibu awape wananchi wake waliomchagua japo walimchagua awawakilishe bungeni  na Bunge lenyewe ni hili lililopo, lakini amegundua halina mvuto ili safari ijayo awape sababu kwanini wamchague tena.”

Mapema wiki iliyopita akiongoza vikao vya Bunge mkutano wa 13 Spika Job Ndugai alifunguka kwa kutaja orodha ya Mawaziri na Wabunge ambao mahudhurio yao ni hafifu kwenye bunge hilo likiwemo jina la Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad