Lipuli FC Ipo Kwenye Wakati Mgumu

Lipuli FC ipo kwenye wakati mgumu
Timu ya Lipuli FC 'WanaPaluhengo' iliyo chini ya Kocha Selemani Matola ipo kwenye haLi mbaya kiuchumi kutokana na kukosa wadhamini.

Habari zimeeleza kuwa mambo ndani ya timu yanazidi kuwa magumu kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa timu kuwa mikononi mwa uongozi.

"Gharama za uendeshaji ni kubwa na hakuna mdhamini kwa sasa hivyo timu inakwenda kibishi na kikubwa sana ambacho tunahitaji ni kupata wadhamini ambao wataipa sapoti hali sio shwari kwa sasa," kilieleza chanzo.

Kocha wa Lipuli, Selemani Matola alisema kuwa wadau wanapaswa wawape sapoti hasa kutokana na hali halisi ilivyo.

"Ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa kuhusu gharama hilo lipo wazi, kwa kuwa sasa hatuna mdhamini mkuu kwenye ligi, wadau watoe sapoti kwa maendeleo ya timu yetu," alisema.

Wachezaji wawili tayari wameondoka ndani ya Lipuli kwa kile kilichoelezwa kutolipwa stahiki zao ni pamoja na Jamal Mnyate na Maalim Busungu ambaye alisema kuwa anahitaji kufanya biashara kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad