Lynn Atoa Baraka Zote kwa Daimond Kumuoa Kim Nana "Ruksa Kabisa Daimond Kumuoa Kim Nana"

Lynn Atoa Baraka Zote kwa Daimond Kumuoa Kim Nana "Ruksa  Kabisa Daimond Kumuoa Kim Nana"
Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia kichupa cha wimbo wa ‘Kwetu’ wa Msanii Rayvanny, Irene Hillary maarufu kama Lynn amefunguka na kusema ni ruksa kabisa Kwa Diamond kumuoa Kim Nana.

Lynn alifunguka hayo siku chache Baada ya warembo hao wawili wanaosemekana kufaidi Penzi la staa huyo wa Bongo fleva kugongana katika shoo ya Wasafi Festival mkoani Mtwara.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa warembo hao ni Kama paka na panya kutokana na wote kumpenda staa huyo hivyo walivyokutana Mkoani Mtwara kila mmoja alipooza na kuonekana wakiangaliana kwa jicho la uhasama.

Kama utakuwa uliwafuatilia walipopanda jukwaani utakuwa uliwashuhudia walivyokuwa wakikatana jicho la ukali.

Lakini Kim anaonekana kuibuka kidedea maana tofauti na Lynn, yeye alionekana mwenye furaha huku akikata nyonga kuashiria hakuwa na stresi kama mwenzake.

Hata wakati wa kurudi Dar, Lynn alipanda gari la wanenguaji na njiani alionekana kabisa hana furaha, tofauti na Kim aliyepanda kwenye gari moja na wanamuziki wa Wasafi na kujitwalia mapozi kama yote hivyo kumaliza kabisa umalkia wa Lynn ndani ya Wasafi”.

Baada ya tetesi hizo za kuwepo wivu wa kimapenzi Lynn alipiga stori na Gazeti hilo na kufunguka kuhusu  mahusiano yake na  Diamond na Kim Nana.

Unajua kuna kitu watu hawakijui kuhusu mimi na Diamond. Mimi na Diamond hatua uhusiano wowote ule.

Diamond ni mshkaji wangu sana kwa hiyo hata akimuoa Kim haiwezi kuniuma kwa sababu atakuwa wifi yangu na nimebariki amuoe tu wala sina tatizo lolote,

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad