Imeelezwa kuwa wajumbe wa muwekezaji, Mohamed Dewji 'Mo' wamepatikana ili kuunda bodi ya wakurugenzi wa Simba, wakurugenzi hao wataungana na wajumbe waliochaguliwa na wanachama ili kuunda rasmi bodi ya wakurugenzi ndani ya klabu ya Simba kutokana na mabadiliko ya uendeshaji.
Wajumbe walioteuliwa kwa upande wa Mohamed Dewji, 'Mo' ni pamoja na Mohamed Nassoro, Hans Poppe, Dr Mohamed Janab, Muslay Lowei, Babla Gonzaranz na Octavian Umshio.
Katiba ya Simba inampa nafasi Mwenyekiti Sued Mkwabi kuteua wajumbe, amewateua Hassan Kapusi na Salim Abdallah 'Try again' ambaye aliwahi kuwa kaimu nafasi ya Rais na aliacha kugombeaa baada ya kusema kuwa amewaachia wengine kupata nafasi.
Wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja na Asha Baraka, Dr Zawad,Hussen Kitita,Seleman Harub na Mwina Kaduguda.