Madereva wa Serikali Nchini Watakaovunja Sheria Kufungwa Pingu

Madereva was Serikali Nchini Watakaovunja Sheria Kufungwa Pingu
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fortunatus Muslim amesema kuwa madereva wa serikali watakaokamatwa kwa kuvunja sheria atawapiga Pingu kisha kuwafikisha mahakamani na wakitoka huko atawaondolea sifa.

Kamanda Muslim ameyasema hayo wakati akiwa kwenye Oparesheni ya kuhakikisha barabara zinakuwa salama na kuepusha ajali ambazo sio za lazima, hasa zinazosababishwa na magari ya serikali ambapo madereva wengi wa serikali wanaonekana wapo juu ya sheria.

“Madereva wengi hamtaki kufata sheria wala alama za barabarani mnaendesha mwendokasi hata mkisimamishwa nyie mnawasha taa, muda mwingine viongozi wanakuwa ndani ya hayo hayo magari na wanalipia faini,” amesema Kamanda Muslim.

Kamanda Muslim ameongeza kuwa, “Sasa hivi tukiwakamata tunawapiga pingu, tunawaweka ndani kisha mahakamani na ukitoka mahakamani naondoa sifa ya kuendesha magari ya serikali uende kuendesha magari mengine".

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa ajali zinazohusisha magari ya serikali na kusababisha vifo vya watumishi wa Umma pamoja na viongozi, miongoni mwa viongozi waliopata ajali hivi karibuni ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ambaye alimpoteza afisa habari wake kwenye ajali hiyo, wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Ofisi ya CAG nao ni wahanga wa ajali hizo mwaka huu.

Mei 24, 2018 Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka mubashara kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, alifunguka kuwa endapo serikali itaendelea kuwafukuza kazi darasa la saba na kuwaajiri 'graduates' kutoka vyuo vikuu ajali hazitaweza kuisha kwani madereva hao wanakuwa na mawazo wanapowaendesha viongozi wenye elimu ndogo kuliko wao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad