IKIWA ni siku moja tu baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza kuwa Serikali itanunua korosho kwa bei ya Tshs 3,300/= kwa kilo moja na zoezi kusimamia Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) huku akipiga Marufuku Uingizwaji wa korosho kimagendo kutoka nje ya Tanzania mapya yameibuka Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, Aziza Mangosongo amemkamata mtu mmoja akiingiza Korosho za magendo kiasi cha magunia zaidi 90 yenye kilo zaidi 100 kila moja kutoka nchini Msumbiji katika maeneo ya mpakani akivusha korosho hizo jana Novemba 14, 2018.
DC Aziza akiwa na Wajumbe Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Newala alimkatama mtuhumiwa huyo wakati wa Operation Maalumu inayoendelea wilayani humo kudhibiti uingizwaji wa Korosho hizo za magendo kama Rais alivyoagiza.
Mhe Aziza amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali kuendelea kufichua vitendo vichafu kutaka kuihujumu nchi na ukiukwaji wa sheria.
Magunia ya Korosho ya Magendo Kutoka Msumbiji Yakamatwa Mtwara
1
November 15, 2018
Tags
Mh haziza na wa Tanzania hapo kuna kazi kubwa kuwatofautisha wamakonde wa msumbiji na Tanzania. Kuna taarifa kuna muingiliano mkubwa Kati yao. Nasikia wapo wengine wanaishi msumbiji lakini wanalima mashamba yao Tanzania na kurudi nyumbani msumbiji baada ya kazi. Pia huduma muhimu hupata Tanzania kama tu watanzania wengine. Huenda hata hili la korosho walijiona na wao linawahusu, maana huenda washazoea kujichanganya na watanzania. Naona wakiwa Tanzania hata bila viza wao hujiona wako nyumbani. Tanzania ni kama nyumba yao ya pili ni kama kwao. Lakini ni watu poa utawapenda ni kama ndugu
ReplyDelete