Maimartha Jesse "Mniache Umbea na Udaku Ndio Kazi Yangu

Maimartha Jesse ‘Mai’

MTANGAZAJI Maimartha Jesse ‘Mai’ amesema kuwa yeye hashtushwi na matusi anayotukanwa na waja wa mtandaoni na wala hataacha umbea kwani ni kazi yake inayomuweka mjini.  Akizungumza na Risasi Jumamosi, Mai alisema kuwa kila akitupia habari yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram watu wanamtukana na kumuita m’mbea, wengine wanadiriki kumwambia auze biashara zake lakini wanasahau kuwa kazi hiyo ameisomea na anahabarisha kama wengine wanavyohabarisha.

“Unajua utangazaji ni sawa na umbea, mimi nahabarisha watu kwa staili yangu na sitokoma kazi hii labda watu wafiche mambo yao lakini hivi hivi sikomi, ni kazi kama kazi nyingine,” alisema Mai. Mai alisema hayo baada ya kuoga mvua ya matusi kutoka kwa mashabiki wa mwanamitindo Hamisa Mobeto pale alipotupia picha ya mwanaume na kudai kuwa ni mume mtarajiwa wa Mobeto.

Mai alitoa picha hiyo kwenye ukurasa wa Snapchat wa mwanamitindo huyo na kuitupia kwake kisha kuandika; ‘Boyfriend wake Hamisa mmemuona… kesi zote za Chibu ameshashtakiwa huyo kijana na wanawake tulivyo hatutaki utani.. Anyway all the best Missa with your new boyfriend





STORI: Hamida Hassan, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad