Majizo Ayakumbuka Maisha ya Lulu Segerea

Majizo Ayakumbuka Maisha ya Lulu Segerea
Mkurungezi wa kituo cha radio na TV ya EFM Majizzo ambaye pia ni mpenzi wa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameikumbuka siku kama ya leo ya November 20,2018 na kusema kuwa itabaki kama kumbukumbu kwake.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Majizzo amesema kuwa siku kama ya leo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamepanga foleni kumuona Elizabeth Michael magereza ya Segerea kipindi anatumikia kifungo chake.

Majizzo amesema pamoja na kwamba Lulu alikuwa kifungoni lakini bado alikuwa akimkuta mwenye tabasamu..>>>“Siku Kama ya leo muda Kama huu nilikua kwenye foleni ya kuingia SEGEREA kumsalimia Mrs Majizzo, Nipofika Ndani nilikutana na Tabasam Kama hilo kwenye picha kutoka kwa @elizabethmichaelofficial…..Kwa mapenzi ya Mungu leo imebaki Kama kumbu kumbu!”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad