Mange Kimambi Ampigia Saluti Alikiba Baada ya Kujaza Show Yake ya Kahama "Hakika Wewe ni Mfalme"

Mange Kimambi Ampigia Saluti Alikiba Baada ya Kujaza Show Yake ya Kahama "Hakika Wewe ni Mfalme"
Mwanadada mwanaharakati Mange Kimambi ambaye ameonekana kuwa na mahaba makubwa na Msanii Alikiba amenyanyua mikono juu na kumpongeza mwanamuziki huyo kwa kufanya bonge la show Kahama bila kiki wala promosheni ya kutangaza show yake lakini amejaza watu.

Kupitia ukrasa wake wa instagramu ameonekana kumpa heshima ya Ufalme na kuwatumia dongo wasafi na clouds ambao walitumia promo nyingi kutangaza matamasha yao huku wakionekana kuleta uhadui mkubwa baina yao.

Aliandika Hivi:

Msanii mkubwa pekeee TZ asiehitaji kiki, wala matusi, wala drama ili ajaze show. Anajaza show kwa kutumia talent yake tu tena bila hata promotion. Ilibidi siku moja apewe tunzo ya heshima na BASATA. Huyu kijana ni mfano wa kuigwa na kila msaniii Tanzania.
.
.
Imagine watu wanatoana macho yeye kimyaaaaa. Na show yake imesell out bila kulumbana na mtu..Wasanii mna la kujifunza kwa mwenzenu. .
.
Na ndo maana Kiba hata akae miaka 5 hajatoa nyimbo hashuki na watu wanakaa wanamsubiri atoe na akitoa nchi inalipuka utasema hakukaa kimya miaka miwili.Ni sababu hana ghasia na mtu. Hana makashkash.
.
.
Congrats Kiba. Hakika wewe ni mfalme maana hata tabia zako za kifalme. Tangu Tanzania iumbwe hajatokea msanii mstaarabu kama huyu. Hail to the King 🙌🙌🙌🙌👑👑👑👑
.
.
.
PS: Hakuna alietajwa sasa mtakaojihisi sababu mnajijua mnatabia zakikum* kazi kwenu......

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad