Mapya yaibuka Ajali iliyoua Saba Dodoma



Dodoma. Majina ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyotokea wilaya ya Kongwa jijini Dodoma ikihusisha magari mawili ya Serikali yametajwa ambao ni ndugu watano wa Naibu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Benjamin Magai.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi katika eneo la Mbande wilayani humo, ambapo watu saba walifariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumza katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Kaimu Mganga Mkuu Dk Ibenza Ernest amewataja waliofariki wote ni wakazi wa jijini Dar es Salaam ambAo ni ndugu wa Magai kuwa ni Grace Masatu, Godfrey Samson, Andrew Lucas, Lucas Magai na Willherimia Magai.

Wengine ni mfanyakazi wa Naibu CAG huyo, George Zakayo na dereva wa gari iliyopata ajali ya ofisi ya CAG, Dickson Kitanda ambaye alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad