Jana November 1, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesafirishwa kwa dharura kwenda nchini Afrika Kusini kutibiwa matatizo ya Moyo na Shinikizo la Damu.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.Wakili Nchimbi amedai kuwa mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mbowe hayupo mahakamani.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala ameieleza mahakama kuwa Mbowe amesafirishwa jana jioni akiwa mahututi kuelekea nchini Afrika Kusini, hivyo nyaraka za usafiri na Matibabu zitawasilishwa kwa barua mahakamani.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri amesema endapo Mbowe akishindwa kuwasilisha vielelezo vya kusafiri na ugonjwa wake atatoa amri ya kukamatwa ili ajieleze kwani ni asifutiwe dhamana.Kesi imeahirishwa hadi November 8,2018.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo, wanatetewa na wakili Peter Kibatala ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji. Huku Peter Msigwa anatetewa na wakili Jamuhuri Johnson.