Mauaji Kigoma: Waziri Lugola Atoa Maagizo Mazito Kwa IGP Sirro


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania, (IGP) Simon Sirro kuwaondoa katika nafasi zao Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo na mkuu wa operesheni mkoa huo.

Akiwa katika ziara ya kutembelea wilayani Uvinza mkoani humo leo Jumapili Novemba 11, 2018, ambapo zilitokea vurugu baina ya polisi na wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na kusababisha vifo, waziri huyo pia ameagiza kuondolewa kwa mkuu wa operesheni mkoa na mkuu wa polisi wa wilaya ya Uvinza.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo kupitia mtandao wa Twitter imesema wengine wanaotakiwa kuondolewa ni mkuu wa intelijensia wilaya na askari wote wa kituo cha polisi Mpeta na Nguruka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad