Mayweather Ataka Milion 345 Kuzupiga na Khabib

BONDIA Floyd Mayweather amefikia makubaliano na mdhamini wa masumbwi, Dana White, kuzipiga na bondia Khabib, lakini katika mtindo wa mpambano wa mchanganyiko wa ngumi na mateke (kick-boxing) chini ya shirikisho la Ultimate Fighting Championship (UFC).

Katika mpambano huo, Mayweather ametaka kupewa kitita cha Dola milioni 150, jambo ambalo mdhamini huyo amelikubali.

Hayo yamefikiwa huko Los Angeles, Marekani, ambako Mayweather alidai kitita hicho akijigamba kwamba: “Hiyo ndiyo njia yangu, sheria zangu.  Mimi ni Floyd ‘Money’ Mayweather!”


             Khabib.

Akizungumza na vyombo vya habari, Dana aligusia pia kuwepo kwa mpambano kati ya mabondia Conor McGregor  na Donald “Cowboy” Cerrone ambayo yatafanyika katika wakati utakaokubaliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad